Revelation of John 1

Utangulizi Na Salamu

1 aUfunuo wa Isa Al-Masihi aliopewa na Mwenyezi Mungu ili awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo ni lazima yatukie hivi karibuni. Alijulisha mambo haya kwa kumtuma malaika wake kwa Yohana mtumishi wake, 2 bambaye anashuhudia kuhusu kila kitu alichokiona, yaani, Neno la Mwenyezi Mungu na ushuhuda wa Isa Al-Masihi. 3 cAmebarikiwa yeye asomaye maneno ya unabii huu, na wamebarikiwa wale wanaoyasikia na kuyatia moyoni yale yaliyoandikwa humo, kwa sababu wakati umekaribia.

Salamu Kwa Makanisa Saba

4 dYohana, kwa makanisa saba yaliyoko Asia:

Neema na amani iwe kwenu kutoka kwake aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, na kutoka kwa wale roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi,
5 ena kutoka kwa Isa Al-Masihi ambaye ni yule shahidi mwaminifu, mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, mtawala wa wafalme wa dunia.

Kwake yeye anayetupenda na ambaye ametuweka huru kutoka dhambi zetu kwa damu yake,
6 fakatufanya sisi kuwa ufalme na makuhani, tumtumikie Mungu wake ambaye ni Baba yake. Utukufu na uwezo ni vyake milele na milele! Amen.
7 gTazama! Anakuja na mawingu,
na kila jicho litamwona,
hata wale waliomchoma;
na makabila yote duniani
yataomboleza kwa sababu yake.
Naam, ndivyo itakavyokuwa! Amen.

8 h“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mwenyezi Mungu, “aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”

Maono Ya Al-Masihi

9 iMimi, Yohana, ndugu yenu ninayeshiriki pamoja nanyi mateso katika Isa na katika ufalme na uvumilivu katika saburi, nilikuwa katika kisiwa cha Patmo kwa ajili ya neno la Mungu na ushuhuda wa Isa. 10 jKatika siku ya Bwana, nilikuwa katika Roho na nikasikia sauti kubwa kama ya baragumu nyuma yangu 11 kikisema, “Andika kwenye kitabu haya yote unayoyaona, kisha uyapeleke kwa makanisa saba, yaani: Efeso, Smirna, Pergamo, Thiatira, Sardi, Filadelfia na Laodikia.”

12 lNdipo nikageuka ili nione ni sauti ya nani iliyokuwa ikisema nami. Nami nilipogeuka, nikaona vinara saba vya taa vya dhahabu, 13 mna katikati ya vile vinara vya taa, alikuwamo mtu kama Mwana wa Adamu, akiwa amevaa joho refu, na mkanda wa dhahabu ukiwa umefungwa kifuani mwake. 14 nKichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu, nyeupe kama theluji, nayo macho yake yalikuwa kama mwali wa moto. 15 oNyayo zake zilikuwa kama shaba inayong’aa, katika tanuru ya moto, nayo sauti yake ilikuwa kama mugurumo ya maji mengi. 16 pKatika mkono wake wa kuume alishika nyota saba, na kinywani mwake ulitoka upanga mkali wenye makali kuwili. Uso wake ulikuwa kama jua liking’aa kwa nguvu zake zote.

17 qNilipomwona, nilianguka miguuni pake kama aliyekufa. Ndipo akauweka mkono wake wa kuume juu yangu na kusema: “Usiogope, Mimi ndiye wa Kwanza na wa Mwisho. 18 rMimi ni Yeye Aliye Hai, niliyekuwa nimekufa, na tazama, ni hai milele na milele! Nami ninazo funguo za mauti na kuzimu.
Kuzimu linalotokana na neno Hades la Kiyunani au Sheol kwa Kiebrania; maana yake ni mahali pa mateso kwa watu waliopotea.

19 t“Basi andika mambo uliyoyaona, yaliyopo na yale yatakayotukia baada ya haya. 20 uKuhusu siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume na vile vinara saba vya taa vya dhahabu ni hii: Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, navyo vile vinara saba ni hayo makanisa saba.
Copyright information for SwhKC